Vinvaleo (pia: Gwenole; Guénolé; Winwaloe, Winwallus; Plouguin, 460 hivi - karibu na Brest, Bretagne, 532 hivi) alikuwa mmonaki anayetajwa kama mwanzilishi wa monasteri ya Landévennec nchini Ufaransa, [1].
Mwanafunzi wa Budok katika kisiwa cha Lavret, aliyapatia sifa maisha ya kimonaki.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu kama kaka zake Jakuto na Gwetnoko.